Siku zote hujitahidi kuonesha kuwa yeye ni mwanaume na sio mvulana mkubwa.
Anajua na kusimamia malengo yake, ngumu kumkuta akiishi bendera kufuata upepo. Na anapenda kile anachofanya.
Mwanaume anayejitambua anaamini anaweza kufanikisha chochote na kwanza kila muda anapaswa kujifunza mambo mapya kwa ajiri ya ukuaji wake.
Husaidia wengine kukua na wala hawezi kuwashusha ili yeye apande. Hawezi kuchukia wale anaowasaidia wakimpita kimaendeleo kwani anaamini mtoaji ni Mungu pekee
Haongei kitu ambacho hakimaanishi . Anaamini kuwa akiongea uongo ataharibu hadhi yake.
Ukiongea nae kila wakati unajifunza kitu, anakufanya ujisikie na ujiamini kuwa unaweza. Vijana wengi humuita rolimodo wao.
Haijlishi kazi au mazingira aliyopo, Atajitahidi awe smart na anukie vizuri no mara waaaaa…
Mwanaume imara, anayejiamini, anayejitambua na kuelewa wajibu wake, hatishwi na uimara wala mafanikio ya wengine.
Mwanaume anayejitambua atafurahi zaid pale anapokosolewa kuliko kusifiwa sifiwa hovyoo.
Hata kama tatizo ni kubwa namna gani hawezi kukimbia, atatafuta mbinu yoyote ya kulitatu hata kwa kushirikisha wengine.
Hata kama akifiwa au mahusiano yake yakivunjika, Humkuti akilia lia au kulalamika hovyo mbele za watu au mwenye mitandao ya kijamii.
Hufanya kila njia mwanamke wake awe na furaha na amani na kumtimizia mahitaji yake yote.
Mwanaume anayejitambua hawezi kucheat, na hata ikitokea kwa bahati mbaya, hatokiri ili kulinda imani na amani ya mwanamke wake kwake.
Sio mtu wa kupenda mzaha na wala sio mtu wa kuomba omba msamaha kila wakati isiyokuwa na kichwa wala mkia.
Mwanaume anayejitambua jamii yake humtambua kwa mchango wake. Hakosi kuhudhuria shughuli zote za kijamii labda awe na dharura. Ni mtu wa wapwa haswaa.