Kuna Mshkaji Yupo Gereza Moja Manyara Amepigwa Miaka 30 Kwa Kubaka Lkn Yeye Anasema Hakubaka


twitter thread from
Kuna mshkaji yupo gereza moja Manyara amepigwa miaka 30 kwa kubaka lkn yeye anasema hakubaka.

Anasimulia; huyo binti hakulala nyumbani kwao siku hiyo(ni mwanafunzi), baba yake akawa anamsubiri kwa hasira, asubuhi kurudi baba yake akamdaka, akaanza kumpiga, binti akaponyoka,

Yeye mshkaji kaamka asubuhi anapiga mswaki nje kwake(nyumba siyo mbali na kwa huyo binti), yule binti baada ya kuponyoka akakimbia, alipoona mlango wa jamaa upo wazi akachoma ndani, jamaa akashangaa, akaingia ndani kuuliza kulikoni na amtoe,
Hajakaa sawa baba yake na binti nae kafika pale, akawafungia mlango kwa nje, jamaa akauliza kulikoni, yule mzee akajaza watu na kusema binti ndipo alipolala. Wakaenda kumpima binti wakakuta kweli kaingiliwa kimwili. Basi ndipo jamaa alipo angukiwa na hiyo TUFANI.
Katika ushahidi binti akakubali kuwa kweli alilala kwa hiyo mshkaji(ili tu amwokoe yule jamaa yake ambako ndiko kweli alikuwepo). Jamaa ndiyo akapigwa mvua 30.

Anasema yeye kishafungwa miaka 30, kama angekuwa kabaka angesema tu sababu tayari yupo gerezani(na askari akiwepo).

Kwahiyo anasema anasubiri kudra za mwenyezi Mungu ndizo labda zitakuja kumtoa.

Dunia ipo katili sana.
MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published.